MP Tanga Urban Constituency 2020 - 2025 & Minister of Health Tanzania🇹🇿 from Jan 2022 to-date | Minister PO - RALG 2021 | Minister of Health 2015 - 2020
Asante sana Prof
@kitilam
kwa kutambua kazi kubwa ya Mhe Rais
@SuluhuSamia
katika kupunguza vifo vya watoto wa umri chini ya miaka mitano na vifo vya wajawazito nchini kwetu. Nakushukuru pia kwa kutambua mchango wangu katika kupata matokeo haya! Pongezi hizi nazirudisha
kwa
Ooh Allah, Thank you for giving me another year, for giving me life. All that I am is because of you Allah, and I bow to you only, Alhamdulillah. It's my birthday🌺
Its my birthday🌺. Alhamdulillah. Namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuongeza mwaka ktk maisha yangu.
Ummy Mwalimu wa sasa Vs Ummy Mwalimu 10 years ago. Ama kweli siku hazigandi.
On this special occasion of my life, I pray for nothing else than the guidance of Allah in everything I do and every path I take. Happy birthday to me!
Pongezi nyingi kwa Vijana wetu wa
@Coastalunion_fc
Hakika mmejituma. Kwangu mimi na wengi nyie ndio washindi wa game la lao. Hongereni sana! Asanteni sana kwa kuiheshimisha Tanga na Soka la Tanga. So proud of you
@Coastalunion_fc
Alhamdullilah! Namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuongeza mwaka ktk maisha yangu. Ninawashukuru wote mlionitakia heri na kuniombea mema. Nami ninawaombea heri na baraka ktk kazi na maisha yenu
#virgowoman
Nb. Kwa wapiga kura wa
#TangaMjini
ni hivi
#odoummyatosha
✅
#Magufuli5Tena
Mimi na mama yangu tunawakia Eid Mubarak!
Mwenyezi Mungu uwalinde na uwape afya njema wazazi wetu na pia uwarehemu wazazi wetu waliotangulia mbele ya haki. Eid Mubarak! Kutoka kwa watu wa Tanga Mjini🙏
A good heart has stop beating! My heartfelt condolences to his family. Mungu awape nguvu katika kipindi hiki kigumu. RIP Balozi Augustine Mahiga. Ulikuwa mtu mwema sana, usie na makuu na kutojikweza licha ya nafasi kubwa/nyeti ulizowahi kushika nchini na kimataifa. PKA Balozi.
Alhamdulillah! Ninamshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema kwa kuongeza mwaka mwingine ktk maisha yangu. Asanteni sana wote mlionitumia na mnaoendelea kunitumia salaam za heri ktk Siku yangu. Mwenyezi Mungu awabariki sana
#VirgoWoman
Suala la mtoto Anna Zambi: Serikali kupitia Wizara ya Afya na
@maendeleoyajami
tunachukua jukumu la kuratibu na kusimamia psychosocial support ya mtoto huyu pamoja na ustawi wake kwa ujumla. Katibu Mkuu Dkt John Jingu leo ataitembelea familia yake iliyopo Goba. Tutatoa taarifa.
Mungu ni mwema. Na leo pia hatuna case mpya za COVID19. Mgonjwa wa Kagera (Ngara) amepona. Sasa jumla ya waliopona ni 3. Mgonjwa aliebaki wa Arusha vipimo vyake siku ya 9 leo ni Negative. Tutampima siku ya 14 ili kujiridhisha kama amepona. Wengine 15 waliobaki wanaendelea vzr
Rest In Peace Senator Ndassa! Mtani wangu! Daima umekuwa ukinitia moyo ktk kazi zangu toka nikiwa Naibu Waziri mwaka 2010 na sasa ktk nafasi hii ya Waziri. Asante kwa upendo wako mkubwa kwangu. Asante kwa utani na urafiki wetu! Pole kwa familia ya marehemu na wananchi wa Sumve.
Asanteni sana kwa Pongezi. Nimesoma maoni na ushauri wenu kuhusu utendaji kazi wa TAMISEMI. Tutayafanyia kazi. Aidha toka kuteuliwa kwangu nimepokea sms nyingi za wananchi kuhusu uendeshaji wa Halmashauri zetu hususan ukusanyaji wa mapato, Utawala na matumizi ya fedha za umma
CCM Tanga Mjini imeamua! Asanteni sana sana wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Wilaya ya Tanga🙏🙏🙏. Nina deni kubwa sana kwenu. Nina deni kubwa kwa wana Tanga.
#TangaMjini2020
Asanteni sana wote mlionitumia Salaam za Heri na Upendo katika mfanano wa siku yangu ya kuzaliwa.
Nimepokea Salaam zenu kwa heshma na unyenyekevu mkubwa🙏. Mwenyezi atujalie umri mrefu wenye heri, afya njema na baraka nyingi. Lots of love🌺🌺🌺
Chuma hichoo! Mwenyezi Mungu aendelee kukulinda na kukusimamia rais wetu mpendwa Dkt
@MagufuliJP
. Tunakupenda na kukuombea kwa Mwenyezi Mungu kila lililo jema rais wetu.
Update on
#COVID19Tanzania
. Samples tested at the National laboratory between 18th - 20th April, 84 new cases in Tanzania mainland and Zanzibar. Total confirmed cases to-date 254. We regret to announce 3 new COVID-19 deaths in Dar es salaam.
Happy birthday
@Eric__Bernard
Mwenyezi Mungu akujalie miaka mingi, yenye heri, afya njema na baraka tele.
Nb. Vipi utaendelea kuwashauri watu humu kuhusu mapenzi?😃🤣
Alhamdullilah! Namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuongeza mwaka mwingine katika maisha yangu! Na wote waliozaliwa tarehe kama ya leo ninawatakia maisha marefu yenye afya njema na baraka nyingi.
#Birthday
🙏
Ni majonzi makubwa kwa Tanzania! Tumuombee Mzee wetu Mhe Rais Mstaafu Benjamin Mkapa apumzike kwa Amani. Natoa pole kwa mke wa marehemu Mama Anna Mkapa, watoto, familia, ndugu, jamaa, marafiki na watanzania wote. Bwana ametoa, bwana ametwaa.
Asante sana H.E
@SuluhuSamia
, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
#Tanzania
kwa kuniamini kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI. Nitaienzi heshma hii kwa kuchapa kazi kwa kasi, weledi, ubunifu na bidii zaidi ktk kusimamia Tawala za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa..
Habari njema - wagonjwa 2 wa COVID19 wamepona. Dar es Salaam - 1 na Arusha - 1. Hivyo sasa Mkoa wa Arusha hauna mtu mwenye maambukizi ya COVID19. Tuendelee kuzingatia maelekezo ya Wataalam wa Afya ikiwemo kuepuka mikusanyiko n/misongamano isiyo ya lazima.
#JikingeWakingeWengine
Siku ya mwisho Bungeni Dodoma. Tuna kila sababu ya kumshukuru Mwenyezi Mungu hadi kufikia siku hii. Tupo tayari kumsikiliza Mhe Rais Dr
@MagufuliJP
ambapo ataelezea utendaji kazi wa Serikali ya Awamu ya Tano kwa kipindi cha 2015-2020. Hakika kazi kubwa imefanyika
#TanoTenaKwaJPM
Vipi hapo, tushushe collabo ya Ummy na MsagaSumu? Nimepata bahati ya kukutana 'live' na mfalme wa Singeli nchini
#MsagaSumu
. Kaa tayari kupokea mchango wake ktk kuimarisha hali ya Lishe TZ hususan kwa wajawazito, watoto wadogo na vijana balehe
#LisheBora
@TFNC_TZ
@elimuyaafya
Mama yetu, Janeth Magufuli. Hatutakuacha peke yako. Tunakuombea kwa Mwenyezi Mungu akupe nguvu na ustahamilivu ktk kipindi hiki kigumu.
#ApumzikeKwaAmaniRaisMagufuli
Corona Inazuilika! Ktk kipindi hiki cha Mlipuko wa Ugonjwa wa Corona ninawahimiza wananchi kuepuka mikusanyiko na misongamano isiyo ya lazima. Tuzingatie umbali wa mita 1 kati ya mtu na mtu. Tuzuie watoto kuzurura mitaani au kisingizio cha kutembelea ndugu
#JikingeWakingeWengine
MWENENDO WA UGONJWA WA CORONA NCHINI
Wizara ya Afya inathibitisha uwepo wa wagonjwa wapya 29 wa COVID-19 nchini. Hadi sasa Tanzania idadi ya Wagonjwa imefikia 88 na wote wanaendelea na matibabu chini ya uangalizi wa wataalam afya.
#ChukuaTahadhari
#Covid19Tanzania
@nyuki_malkia
Tafadhali tusaidie jinsi ya kumpata mtoto huyu. Au aelekezwe kwenda moja kwa moja Ofisini kwa Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma (General) kwa ajili ya kupatiwa matibabu.
Anaweza pia kupitia Ofisini kwa Mganga Mkuu wa Halmashauri au Mganga Mkuu wa Mkoa wa
Leo nimechukua na kurudisha fomu ya kuomba ridhaa ya
@ccm_tanzania
kupeperusha bendera ya CCM ktk kugombea nafasi ya Ubunge wa Jimbo la Tanga Mjini. Nitumie fursa hii kuwashukuru wote ambao wamekuwa wakinitia moyo na kuniombea heri ktk mchakato huu
#TangaMjini2020
Hakika jambo hili ni zito na kubwa kulipokea😭😭😭
Ohh Jemedari wetu, Rais wetu Dkt JPM utabaki ktk mioyo yetu kama Rais jasiri, shupavu na uliejitowa kwa ajili ya maendeleo ya Tanzania na watanzania hususani wa kipato cha chini. Pumzika kwa Amani Baba.
#WomenInspiringWomen
- 👍Dr Constansia Buretta amehitimisha mafunzo ya miaka 5 ya Upasuaji wa Ubongo, Mgongo na Mishipa ya Fahamu (Neurosurgery), Chuo Kikuu cha Kagoshima, Japan. Hatua hii inafanya idadi ya madaktari wanawake wenye utalaamu huo (Neurosurgeons) Tanzania kufikia 4
Kuanzia kesho tar 17 April tunatumia Vikundi vya kijamii ktk mapambano dhidi ya
#COVID19Tanzania
.Kwa siku 20 vitazunguka ndani ya Jiji la Dar es salaam kutoa Elimu kwa jamii kuhusu Corona.Lengo ni kukata mnyororo wa maambukizi ya Corona TZ
@elimuyaafya
@trcs1962
@UNICEFTanzania
Natamani ningepata maneno mazuri zaidi ya kumshukuru Mh Rais kwa heshma kubwa hii. Hata hivyo nimekosa maneno hayo zaidi ya kusema "Ahsante sana Mhe Rais Dkt
@MagufuliJP
". Namshukuru kwa kunijenga, kuniimarisha na kunifundisha kutokata tamaa.Ninamshukuru Mwenyezi Mungu kwa hili🙏
“Namshukuru Mungu kuiepusha Tanzania dhidi ya corona, kwa namna ya pekee nampongeza Mwana-Mama Jasiri Waziri Ummy Mwalimu kwa uvumilivu wake, nilimtesa sana Ummy maana nilikuwa nampigia simu mara nyingi hadi saa 8 usiku, naomba aniombee msamaha kwa Mumewe”-JPM
#MillardAyoBUNGENI
Asante sana Rev. Eliona Kimaro, KKKT Kijitonyama kwa kutuombea na kututia moyo🙏! Hakika mnatupa nguvu ya kuendelea kupambana dhidi ya adui Corona. Naomba msichoke kuiombea nchi yetu, kuwaombea na kuwatia moyo watumishi wa Afya walio mstari wa mbele ktk mapambano haya
#COVID19TZA
Asante Mh
@DocFaustine
kwa Utumishi wako na ushirikiano mkubwa ulionipatia ktk kusimamia Sekta ya Afya nchini. Kila la heri ktk kuwatumikia wana Kigamboni. Hongera Dr G. Mollel, Karibu
@wizara_afyatz
na
@maendeleoyajami
. Naahidi kukupa ushirikiano ktk utekelezaji wa majukumu yako
Nimepokea uamuzi wa Mhe Rais kwa unyenyekevu mkubwa. Ninamshukuru sana JPM kwa kunipa fursa ya kuhudumu katika Serikali yake. Nawashukuru sana
@umwalimu
na watendaji wote kwa ushirikiano walionipatia.
Mafanikio ya sekta ni makubwa sana. Namtakia kila la kheri NW ajaye Dkt Mollel.
Kuhusu suala hili - Timu ya Usimamizi Afya ya Mkoa (RHMT) wa Tabora na ya Halmashauri (CHMT) ya Wilaya ya Uyui wanafuatia suala hili.
Serikali itatoa Taarifa kwa umma juu ya hatua zilizochukuliwa. Tunawashukuru wote walioibua suala hili.
Asanteni sana wote mlionitumia salamu za heri na upendo katika siku yangu ya kuzaliwa tar 5 Septemba. Hakika nimeelemewa na upendo wenu mkubwa mliouonyesha kwangu.
Namuomba Mungu atujalie sote umri mrefu, afya njema na baraka nyingi. Asanteni sana 🙏🙏🙏🌺🌺🌺
Kaka yangu, kiongozi wetu Balozi John Kijazi hivi ni kweli umeondoka??😭😭😭 Tangulia kaka. Binafsi nitakukumbuka kama kiongozi mweledi, muungwana na mnyenyekevu kwa kila mtu.
Pole kwa familia na ndugu wa marehemu, Rais
@MagufuliJP
, Watumishi wa umma na watanzania wote. RIP Kaka
Nimepokea Taarifa hizi kwa masikitiko makubwa. Tayari Baraza la Wauguzi na Wakunga Tanzania linachunguza suala hili. Endapo tuhuma hizi zitathibitishwa tutatoa adhabu kali kwa wanataaluma hawa ikiwemo kuwasimamishia au kuwafutia kabisa usajili wao.
It is with deep sympathy that I announce the first death resulted from
#COVID19
; a Tanzanian male, aged 49 years who had other underlying health conditions. Our condolences to his beloved family, relatives and friends. May his soul rest in eternal peace
#COVID19Tanzania
Nimekagua fomu za wagombea wote wa Ubunge Jimbo la Tanga Mjini. Nimebaini makosa ltk fomu za wagombea wengine. Sasa nasubiri majibu ya pingamizi nilizowawekea wagombea walioteuliwa.
#TangaMjini2020
Asante Mhe Rais Dr
@MagufuliJP
kwa kuendelea kuniamini na kunitia moyo ktk kusimamia sekta ya Afya nchini hasa ktk kipindi hiki cha mapambano dhidi ya
#COVID19
. Naahidi kuendelea kuitumikia nchi yangu kwa bidii,uaminifu na maarifa zaidi.
#CoronaInazuilika
#JikingeWakingeWengine
“Nakupongeza sana Ummy najua nilikutesa, sitaki kueleza sana, kwa siku mara nyingine Ummy alikuwa anapigiwa simu zaidi ya mara 8, lakini ndio hivyo, unapokuwa kwenye vita saa nyingine kubembelezana hapana, lakini Ummy unachapa kazi nakupongeza kwelikweli”-JPM
#MillardAyoUPDATES
Mufti wa Tanzania na Sheikh Mkuu Abubakar Zubery ametangaza kuwa kesho Jumapili May 24 ni Sikukuu ya Eid El Fitri baada ya kuandama kwa mwezi katika Mkoa wa Singida. “mimi kama Mufti wa Tanzania na Sheikh Mkuu,nimeuthibitisha mwezi huu ambao umeandama Singida"
(📹via Channelten)
Moja ya mzazi alietutumia sms kuwa kijana wake kachaguliwa HGK wakati kijana alijaza CBG. Tumerudi kwenye mfumo.
Chaguo la 1 ni HGK shule Madibira
La 2 ni HKL Mara sek
La 3 ni HGL Kigwe
La 4 CBG Same na
La 5 HGE Kibiti
Mfumo umempatia chaguo lake la kwanza.
#UchaguziForm5
..3/3
RIP Mama yetu, Askofu Getrude Rwakatare. Upumzike kwa Amani. Mbele yako, nyuma yetu. Natoa pole nyingi kwa familia ya marehemu. Mwenyezi Mungu awatie nguvu ktk kipindi hiki kigumu. Pole Mh Spika wa
@bunge_tz
kwa kupoteza mbunge. Pole kwa waumini wa Kanisa la Mlima wa Moto.
Sijui ni Halmashauri gani hii? Hakika Mtumishi huyu anapaswa kupongezwa. Nimemuelekeza Katibu Mkuu Afya wamtafute. Lkn pia nasi viongozi tunapaswa kufanya kitu ili kuboresha mawasiliano kuwezesha wananchi kupata huduma za afya.
Alhamdulillah! Baada ya kumshukuru Mwenyezi Mungu, ninaishukuru Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) chini ya Mwenyekiti makini Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuniteua kuwa Mgombea Ubunge wa CCM Jimbo la Tanga Mjini ktk…
UTEUZI maDC: Hongereni wote walioaminiwa na Rais Mh
@SuluhuSamia
ktk nafasi ya Ukuu wa Wilaya. Ni matumaini yetu kuwa mtaifanya kazi hii kwa kasi, bidii,ubunifu na uaminifu kwake na kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Karibuni Ofisi ya Rais TAMISEMI.
#KaziIendelee
@ortamisemitz
Kuhusu tetesi za uwepo wa
#COVID19
; Nawaomba wananchi muondoe hofu. Tunachakata taarifa tulizokusanywa kutoka Hospitali/Vituo mbalimbali ndani ya wiki hii...tutatoa taarifa kama kuna ongezeko la magonjwa ya mfumo wa hewa au la??
Kocha wa zamani wa Yanga SC na Polisi Tanzania Mwinyi Zahera Raia wa Congo DR ametangazwa kuwa Kocha Mkuu mpya wa Coastal Union ya Tanga kwa kipindi cha mwaka mmoja.
#MillardAyoSPORTS
Corona ipo lakini magonjwa mengine pia yapo! Tutaendelea kuhakikisha huduma bora na salama kwa magonjwa yote katika vituo vyote vya kutoa huduma za afya - vya umma na binafsi
@wizara_afyatz
“Utafiti uliofanywa na Serikali, katika kila Watanzania 100, Watanzania tisa wana matatizo ya kisukari, akija Mtu wa kisukari apate huduma usianze kumuambia nenda kapime corona, hatuwezi kuacha huduma zisitolewe kisa corona, maisha lazima yaendelee”- UMMY